Tuesday, March 13, 2012

JOS MTAMBO+BELLE 9-NAONGEA NA ROHO 2012

Oiii Peeps!!!!!
Tongwe  Records now comes up with Jos Mtambo ''The Legend of Kigambonino''  featuring Belle 9 in the track NAONGEA NA ROHO
Jos Mtambo talks to the souls of the brothers and sisters we lost.These were very influential people  in East Africa such that would they be alive today
much would be accomplished.Jos pays tribute to these people and remembers their effort in making E.A the place to be.We salute them all and respect their contribution.
JOAS MTAMBO+BELLE 9-NAONGEA NA ROHO
PEACE
J-MURDER
CEO
TONGWE RECORDS

Monday, November 14, 2011

ITS G.NAKO ONCE AGAIN-ROUND HERE 2011

G.NAKO wakundi la NAKO2NAKO SOLDIERS amesha dondosha another track titled “ROUND HERE” ikiwa imefanyika NOIZMEKKAH under DX,hii ni club single out of the official mixtape ya HANGOVER YA HASIRA ambayo itatoka atapokamilisha maelewano na mdhamini wake wa usambazaji na uzinduzi.
G.NAKO-ROUND HERE

Friday, November 11, 2011

IF YOU ARE A MOTHER...KNOW THAT U R "THE GUARDIAN ANGEL"-SYD 2011

SYD an artist from Nairobi Kenya representing OGOPA
DEEJAYS studios,has recently dropped a new song GUARDIAN ANGEL featuring WYRE (da luv child)…produced by Ogopa both audio and video....taliking to UJAZO…SYD said…”the song appreciates All SINGLE MOTHERS and MOTHERS in General...They are truly one in Millions....I salute you all!!!!

Thursday, November 10, 2011

SAUTI YA JOGOO ON STREETS IFIKAPO 26-11-2011

Tarehe 26 mwezi wa 11-2011, CD yenye nyimbo 18 itapatikana katika baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam na mikoani pia. kwa kuanzia sehemu ambazo tumepata ruhusa ya wamiliki kuwa kama sale points ni: Zezzou Fashions (tegeta,afrika sana na victoria), Ufishi super market (sinza-mori),Mctemba investment Tabata-baracuda,  B.E.T outfit mwenge, Etam fashions - Arusha, Zai-fashions, NSSF building Mwanza, Boom explosion records-kishamapanda Street karibu na Hotel Delux Mwanza. Bado tunaendelea kuwasiliana na sehemu mbali mbali za mkoa mingine kama Dodoma, mbeya na kadhalika na tutawahabarisheni maeneo ziada.

Wednesday, November 9, 2011

MWANA FA+LINNAH-YALAITI 2011

MMMMMMMMH…I’M SPEECHLESS…
DOWNLOAD IT IN HERE

RETURN OF THE REAL...BOU NAKO+NARX-ISH KAMA HIZI 2011

Bou Nako toka kundi la NAKO2NAKO soldiers yupo katika harakati nyinginezo za kuendesha maisha lakini mziki upo kwenye blood,hii inadhihirishw na kazi yake mpya alomshirikisha mwanadafada narx.pini linaitwa"Ish kama hizi" ikimaanisha "mambo kama haya",ambayo ni hiphop joint inayozungumzia zaidi hustling za machizi na jamii inavyopotoshwa na siasa danganyifu kila leo,hali ya maisha kuwa duni na hiphop kuwa njia ya ukweli katika kukomboa fikra zetu vijana" 


DOWNLOAD IT HERE

THE PRODIGAL MIXTAPE IS ON THE WAY...

The Prodigal mixtape, Cannibal featuring Prezzo, Bobby Mapesa,UB,Sharama and many more is soon to be in stores near you,,,itakua matata,,,kifaa cha kwanza kutangulia toka Cannibal ahamie Nairobi ili kufanya mambo sawa kwaajili ya mashabiki wake, misumari kumi na tatu,,,its not to miss,,,
call 
 +254729990851 begin_of_the_skype_highlighting            +254729990851      end_of_the_skype_highlighting +255787276352 begin_of_the_skype_highlighting            +255787276352      end_of_the_skype_highlighting or send us an email via ruffystuffy@yahoo.com

Tuesday, November 8, 2011

BONGO FLAVA MPAKA CONGO...HERE IS "SELF KUWA"


Self Kuwa means Self Be, Kuwa is a Swahili word that means Be. I’m

originally from Uvira, D.R.C, now doing my thing in Louisville,
Kentucky. My love for Hip Hop began at the age of 14 after being
introduced to Hip Hop by my Cousin (Raymond) it started off as just
love for the music. In February 2009 the Americana community Center
open a Hip Hop class where we talk about Hip Hop in general, Record
Original Songs and that’s where I met local Dj/Producer Yared also
known as Yaredsound and the metaphysicians of Hip-Hop CPHR DVN who
taught me a lot of things about writing Lyrics. At the age of 16 I
began to write my own lyrics to my favorite beats and 10 months later
I released my first Mixtape Title ‘’The Beginner Boy’’ . Couple things
that separate me from other artists is that when I write my lyrics in
English or Swahili I always try to stay positive, do my best and never
want to imitate other artists, I just want to do me and what’s right
for my community. Artists that inspired and influenced me are Talib
Kweli, K’naan, CPHR DVN, Sugu aka Mr II, Professor Jay, X Plastaz, Fid
Q, Mwana Fa, Madee & LBT. Follow me on Facebook, twitter @selfkuwa,
for more info about what I’m working on.

DOWNLOAD HIS SONG HERE

Sunday, October 16, 2011

CMB PREZZO ADONDOSHA-4 SHO....4 SHIZZLE

Anaitwa Jackson Makini aka CMB PREZZO kutoka nchini Kenya kwa mara nyingine tena amedondosha dude jipya 4 SHO 4 SHIZZY akimshirikisha ULOPA ambaye ndiye producer wa dude hii kupitia studio ya SAMAWATI nchini Kenya…Video ya kazi hii ameshoot na kampuni ya BOOMBA Video inatarajiwa kutoka baada ya wiki mbili katika vituo vyote vya Tv all over  Africa

Saturday, September 17, 2011

TK NENDEZE+JOH MAKINI-AWAY(2011)

“They say i am a very conscious person, i speak my mind through my music. Music is me and i am music...

THE RETURN OF THE DANCEHALL KING-MARK 2 B aka SIMBA

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kupitia mikasa kibao katika life yake…hatimaye mteule halisi SIMBA amerejea na track mpya yaitwa TAKE OVER akimshirikisha KREAGARL….download na uisikilize…

Monday, September 12, 2011

HII NI NYINGINE TENA...ANTIVIRUS VOL-2 (2011)

FOLLOW THE LINK BELLOW TO DOWNLOAD YOUR COPY

Tuesday, September 6, 2011

VATOLOCO SOLDIERS-SITUATIONS(2011)

Kundi la hiphop toka arusha,Vatoloco soldiers wakiongozwa na FiDO
wanakuja na brand new track toka noizmekah inayokwenda kwa jina la
"situations",ngoma inayozungumzia maisha na uhalisia wa msoto ndani ya
mtaa,"hiphop ndo  maisha yetu everyday na revolution goes on and
on,Mafans wategemee album yetu ya "Ungalimi to Queens" hivi
karibuni",asema FiDO.Kama kawaida chrus hapo kasmamia Lavosti na verse
ya pili Ibra da Husla,Verse ya tatu kakanyagia "Bobray"...Harakati
zingine mbali na kurecord audio za kumalizia album ni video shooting
ya nyimbo kadhaa na leo 2namalizia video ya "Situations" chini ya
camera za hoodpixx kwa usimamizi wa m2 mzima DEFXTRO wa noizmekah..
DOWNLOAD IT HAPA>>>

Sunday, July 24, 2011

JOSEFLY+HUSSEIN MACHOZI-SIKUTAMANI

SAJNA AND JOSEFLY
Huu ni wimbo wa crew member wa Tetemesha records anaitwa JOSEFLY, yeye yupo kama mwandishi (mtunzi) rasmi wa tetemesha records lakini pia ni msanii. ndie alieshirikishwa katika wimbo wa Sajna "MGANGA" na pia alihusika katika kuuandika wimbo huo wa mganga, pia amehusika katika utunzi wa wimbo wa msanii mpya C-sir Madini "Kifungu Huru".

So huu ni wimbo mpya wa Josefly ambao kamshirikisha Hussein Machozi. 

SONG'S DETAILS:
Track Name: SIKUTAMANI
Artists: JOSEFLY FT. HUSSEIN MACHOZI
lyrics composed by: JOSEFLY
arranged by: JOSEFLY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Saturday, July 23, 2011

FIDSTYLE ON CHEUSI DAWA TV IS BLAZIN'HIGH!!!

LANGA aka RAISI WA MATEJA ON CHEUSIDAWA TV...
ONE THE ICREDIBLE ON CHEUSIDAWA TV...
KALA PINA ON CHEUSIDAWA TV...


Saturday, July 9, 2011

KAULI TOKA MOYONI MWANGU-JOSEPH MBILINYI

TAARIFA KWA UMMA
Jana tarehe 8 Julai 2011 Polisi walinikamata kwa kile walichokiita kuwa ni kufanya mkutano bila kibali.Hata hivyo, mtiririko wa matukio unaonyesha kwamba polisi walisukumwa na sababu nyingine kwa kuwa suala la taarifa kupelekwa polisi kama sheria zinavyohitaji lilishashughulikiwa na viongozi wa CHADEMA mkoa na wilaya ya Mbeya Mjini.
Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘BURUDANI NYUMBANI’) ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la FIESTA pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.
Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa RUANDA NZOVWE ambao ni maarufu kama Uwanja wa Dr Slaa wakisubiri tamasha hilo lakini polisi wameonyesha dhamira ya kutaka kuwatawanya.
Maneno na vitendo vya Jeshi la Polisi vinaelekea kuwa na uhusiano na kauli ambayo niliitoa hivi karibuni kupitia mtandao wa Facebook ya kutohitaji tamasha la Fiesta kufanyika Mbeya.
Katika mazingira haya ni muhimu nikaeleza tu kuwa kauli yangu kuhusu Fiesta ilikuwa na madhumuni ya kuanzisha mjadala kuhusiana na suala zima la wizi na unyonyaji uliopo kwenye Sanaa, ambao sio tu unawanyima haki Wasanii, bali pia kukosesha mapato kwa Serikali ambayo  yangetokana na kodi  kupitia Sanaa ikiwemo muziki.
Nilifanya hivyo baada ya tamasha hilo kutangazwa kufanyika katika eneo ambalo wananchi wamenipa wajibu wa uongozi wa kuwatumikia na kuwawakilisha. Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Mbeya Mjini wanaokosa mapato katika sanaa na wasanii wa Mbeya wanaokosa fursa kutokana na vikwazo nilichukua uamuzi wa kuwakilisha kupaza sauti kama ambavyo nimekuwa nikipaza sauti katika masuala mengine yanayogusa umma kama viwanda, kilimo, barabara za Mbeya Mjini na Haki za wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na makundi mengine katika jamii.
Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi  ni sehemu ya vyanzo vya maovu  kwenye maendeleo ya  muziki hapa nchini.  Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa.  Na hii ni kutokana  na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise) biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi  watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye  biashara ya muziki.
Waandaji  wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.
Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa.  Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye  Tamasha la  majahazi, Zanzibar.  Lisingekuwa jambo baya kama wangetumia nafasi hizo kwa haki na maendeleo ya sanaa.  Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya (“empire”) hii imetumia nafasi yake dhalimu  kukandamiza watu wengine hasa Wasanii.   Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo “himaya” yao basi hana nafasi ya kutimiza ndoto yake.  Na iwapo Msanii hakubaliani na taratibu zao au malipo finyu wanayowalipa Wasanii, basi watahakikisha wanampiga vita na hatimaye kuhujumu usanii wake ili atoweke, kwa kuwa tu  hakubaliani nao.  Msanii hana haki ya kufanya majadiliano ya kibiashara mbele yao.
“Empire” hii imehodhi mpaka  makampuni ya udhamini hapa nchini, ambapo makampuni haya yamekuwa magumu kutoa udhamini kwa wadau wengine kwa kuwa tu wao ni washirika wa “Empire” hii.
Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa “Wadosi” ambapo bila ya wao kuruhusu basi  Msanii yeyote kazi  yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika.  Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.
Kibaya zaidi wamehodhi mpaka  nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii.  Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii wa Tanzania, lakini baadaye  tukashangaa kusikia ipo mkononi!  Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini yao na ndio  makao ya THT!  Wamefanikiwa kumhadaa Rais kuwa wao ndio “Care takers” wa Sanaa ya Tanzania akawaamini na wao wanaitumia vibaya imani njema ya Rais kwao kufanya dhuluma.  Yote niliyoyataja juu,  japokuwa hayo ni kwa uchache tu! Yanalalamikiwa sana na wasanii wengi na  wadau hapa  nchini, japokuwa wengi wameshindwa kujitokeza waziwazi kutoka na vitisho vya watu hawa.
Vitendo hivyo wanavyofanya vimeleta madhara katika tasnia ya sanaa na   matokeo yake ni kudumaa kwa maendeleo ya muziki hapa nchini.  Vijana wengi wanaojihusisha na sanaa wamepoteza matumaini.  Wengi walipata tegemeo la ajira kupitia muziki, lakini hali haipo hivyo tena.  Vijana wengi wasanii wamekata tamaa kwa ajili ya ukandamizaji wa “empire” hii.
Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili.  Kwa watu  hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi.  Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa UDSM, hata katika hali hii mbaya ya biashara ya muziki, Serikali imepoteza Tsh. Milioni 18, kwa kutokusanya kodi kupitia muziki tu, ukiachilia mbali filamu na sanaa nyingine.  Na iwapo hali itaboreshwa basi kodi hiyo itapanda mpaka wastani wa Tshs. Bilioni 50 kwa mwaka!  Hizi sio pesa kidogo kwaserikali, hasa ukizingatia bajeti ya Wizara inayohusika na Utamadnuni ni Tsh bilioni 14, kwa mwaka,  fedha ambazo mara nyingi hawapewi zote kutokana na Serikali kutokuwa na fedha ya kutosha! Lakini hapa utaona kukwa kodi ya mwaka peke yake ingetosha kwa bajeti ya Wizara na ziada kubwa ingebaki kwa miradi ya maendeleo kama kujenga Art Theatres n.k
Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni “Mhanga” au “victim” wa uharamia wa “himaya” hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama mwakilishi umma.
Izingatiwe kuwa  baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa  kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge.  Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi.  Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria walianza kulipwa vizuri kama wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.
Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira,  Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?
Wenu katika kutaka haki,
Joseph Mbilinyi (Mb)
9/7/2011-Mbeya Mjini

Tuesday, July 5, 2011

CHEUSI DAWA TV...YANIPA MZUKA WA "CYPHER"...PPPUUUFFF!!!

FID Q...THE HOST OF FREE STYLE ON CHEUSI DAWA TV...
ZAIID FROM KWANZA UNIT...LIVE ON CHEUSI DAWA TV
STEREO FROM LUNDUNO...LIVE ON CHEUSI DAWA TV...
NIKKI MBISHI FROM LUNDUNO...LIVE ON CHEUSI DAWA TV...

Friday, June 24, 2011

STOP IT HATERS...NONINI IS GOOD AND CLEAN

POTRAYED NEGATIVE IMAGE FOR ‘NONINI’
We are saddened by the recent articles published in one of the tabloids on 7th June 2011 in relation to the public character of the above artist ‘Nonini’ It was portrayed that the artist is a violent person and that he was involved in a fight at the Rangers restaurant during an evening out. The artist named is not a violent person; neither did he get involved in a fight at the said restaurant. Witnesses at the venue can counter for every detail that happened that night.

We are thus saddened that an Editor of a renowned magazine plus their reporters can publish such lies and insults. Morever, this story led to reputation damages to Nonini and on his brand. Nonini is currently working on final touches for his movie “Killer moja” which will be released hopefully on 2nd October, 2011. The above matter has in one way or another affected the execution of the above project.

Thursday, June 23, 2011

mo PLUS+JOH MAKINI-X RAY VIDEO IS DONE SHOOTING

MOPLUS na JOHMAKINI ndani ya video ya X-ray ilofanywa chini ya camera za hoodpixx arachuga kwa uongozi wa producer/director DeFXtro,Track inayopatikana ndani  ya "babawa ukoo" Vol 1 album iiliyo kitaa tayari kwa shillingi elfu  tano za kitanzania holla…
@ +255 715 240 005 
HIP HOP…..SOMETHING TO TALK ABOUT

NANI KULINYAKUA TAJI LA VODACOM MISS MWANZA 2011 LEO???

IT ALL ENDS TONIGHT AT GOLD CREST HOTEL….
DIANA JOSEPH-20 YEARS
EIZA RISHARD-20 YEARS
ELIZABETH ZACHARIA-21 YEARS
ESTHER LAWRENCE-22 YEARS
IRENE KARUGABA-21 YEARS
JEALO LAZARO-20 YEARS
JESCA INNOCENT-19 YEARS
JUDITH JOHN-20 YEARS
LUCY LEWIS-20 YEARS
MONICA JAMES-22 YEARS
NEEMA EDMUND-21 YEARS
SABRINA HAMADI-22 YEARS
SEMENI STEPHEN-20 YEARS
STELLA CHARLES-21 YEARS
ZUWENA MSEKWA-20 YEARS

                MISS MWANZA
DATE:-24-06-2011
WAPI?:-GOLD CRREST HOTEL MWANZA
KIINGILIO:-20,000 V.I.P na 10,000 seat za kawaida
PICHA ZOTE ZA WASHIRIKI NI KWA MSAADA WA http://thebigtopten.blogspot.com/ 



































Template by:
Free Blog Templates