ROMA
INTRO…..
Yeeeah waacheni watoto wadogo waje kwangu….
Maana ufalme wa mbinguni ni wao
j..ryder where you ‘t?
am the pastor of this church(times 2)
am the…….it’s tongwe records
VERSE….1
Fanya ishara ya msalaba upokee haya mahubiri
Mimi ni mteule ninawaletea injili
Nina ushuhuda wa kiroho bwana yuaja msubiri
Natangaza upako na habari za mnara wa babeli
Wachungaji wanalumbana wakigombania waumini
Wanalala…wakiamka wanaanzisha dini
Hawaogopi damu ya msalaba bible wanaifanya biashara
Wewe sio yesu hata kama baba yako ni fundi seremala
Wewe ni nani usiyekosea kila unaye muombea anapona
Hatutaki shuhuda za uwongo aminini nyote mtachomwa
Ndani ya vazi la suti unakebehi wakatoloki
Mtaleta dini zote ila RC itabaki
Hata kristo alipoponya hakutaka malipo
Akaunti yako imejaa sadaka zetu wakristo
Toba yako haijaswii halafu unajiita una upako
Siyo kila atakaye niita bwana basi ataiona pepo
CHORUS….
We ni nani unayejiita nabii kwenye jamii
hizi nyakati za mwisho soon atashuka masihi
piga magoti tusaaaaliii !!! Ameeen…..!!!
piga magoti tusaaaaaliii !!!Ameeen….!!!
Waumini wamekimbia kanisa madhehebu yanaongezeka
hizi nyakati za mwisho cheki manabii wa uwongo
mwana wa adam yuaja…. Ameen !!!
mwana wa adam yuaja …Ameen!!!
VERSE…2
Laiti ningeweza ningekugeuza jiwe la chumvi
Vipi unipangie sadaka pastor gani we mlanguzi
Hakika ilinenwa usitumikie mabwana wawili
Siasa na kanisa kama hadithi za kaini na abeli
Kama wasabato wasiokula kitimoto wala kambale
Wanasadaki mbele ya haki wanaamini agano la kale
Mnatangaza ufahari wenu kwenye vikapu vya sadaka
Hakuna sadaka ya kweli kama ya kumchinja isaka
Kanisa lako halifanani na ufalme wa yehova
Madhehebu yanajitenga kama makundi ya bongo fleva
Heshima ya mkatoliki inashuka kama theluji
Dini mnaifanya miradi kwa kivuli cha uchungaji
Kanisani mnaonyeshana ufahari wa kuvaa bazee
Hekalu mnalichafua kwa sadaka ya pedeshee
Biblia hujaimaliza unataka uzima wa milele
Usije ukatuchoma moto kama wafuasi wa kibwetere
Verse…3
Hizi nyakati za mwisho soon atashuka masihi
Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii
Kukataza waumini wasivae mapambo kwako jadi
Ili pesa wakupe sadaka na kisha unafanya mtaji
We mchungaji umekusanya waumini kwenye vijiji
Ukawaongoza sala ya toba kama yohana mbatizaji
Unabeba gunia la dhambi na yesu kumvika taji
Usiniwekee mkono kichwani huna karama ya uponyaji
Imani yako ndogo kama punje ya haradani
Uza mali zako zote pesa uwape masikini
Unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa
Haleluya haleluya kumbe unatuibia sadaka
Yesu hakuwa mganga wa kienyeji Japo alimponya kipofu
kwa tope la mate yake ila kwako napata hofu
ee mungu napiga goti hiki kikombe kiniepuke
mwana wa adam yuaja basi tungoje ashuke
OUTRO
Angalieni mtu asiwadanganye…maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema
“mimi ni kristo” nao watadanganya wengi haleluya…!!! Ameeen….!! manabii wengi wa uwongo watatokea, kutakuwa na dhiki kubwa siku hiyo…jee hamsadiki yakuwa hizi ni ishara kwamba mwana wa adam yuaja…..Ameeen!! basi kesheni mkisali maana hamjui saa wala siku
Am the pastor of his church…am the….its tongwe records…..
0 comments:
Post a Comment
DEE BᵘᵐZ®