Monday, September 27, 2010

UKISIKIA PAAAAAH...JUA IMEKUKOSA>>>LYRICS

JCB,FID Q,JAY MOE,CHIDI BENZ

Intro
ahhh...ahhhh
ohhh yeahhh..(shhhh!).. it's the remix
(shhhh!)...JCB....(ahhhh!).....Murder..!
(Tongwe Records Babyyyy)
VERSE 1 (JCB)
Damu ilitapakaa baada ya ule mlio kulia PAAA,
Watu wote walisambaa hata walevi wa kwenye bar,
Sio polisi sio baunsa iliye kaa utashanga kwa nini mshkaji alizidi kumimina kwa kujiamini,
Amini usiamini akabaki tu na mimi,
Akanishikia bunduki kwa chini,
Akadai eti nimpe madini lasivyo ananipiga risasi kama sabini,
Anasura kama idi amini akarudi karibu atua tatu mpaka kabatini,
Akatamka HEYOO! nipo kazini nimetumwa mzigo au ujithamini,
Akanikanyaga kwa chini kikorofi bunduki tena akaikoki
Akasema kama simuonyeshi leo sio koki,jinsi alivyo akilenge ye akosi mikosi,
Kavaa koti jeusi jasusi,
Mikono nikaweka juu kuepuka nukx huku natukana mengi matusi...
Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
VERSE 2 (FID Q)
Wanasema hugeuka mnyama sana anaposaka pesa
Cha ajabu anavuta bangi lakini hawazii magangstar
Hampaki rangi donkey ili ageuke kuwa zebra
Ndo maana kabla hajaikoki, JCB ali-surrender
Akajifanya hayuko na mie ili niipigie defender
Nikaona vipi nijistukie ghafla nikasikia ''RASTA''
Jambazi linaniita halafu sioni wakuni-backup
Hali inatisha sikuongea nilishut the fluck up
Akaniuliza.. we sio Fid Q yule anayeheshimika mtaani ?
Nikamwambia ndo mimi na huu ndo muda wa kumlaani shetani
Sie wote ni watoto wa mjini siamini vipi hatujuani
Mie alwatani kama Kwere au Chindo popote amani
Akaniambia.. waambie machizi i'm sorry, leo mna-rap wapi ?
Mie sio mtu wa stories, i make things happen
Hii sanaa ni ya watengwa na ngosha...
Ukisikia Paaaaaaaa........ ujue imekukosa
Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
VERSE 3 (JAY MOE)
(aahhh!) Alipogundua ni wasanii,haraka haraka akatuacha
Ndipo tulipomsihi,na watu wengine kuwaacha
Maana ishakuwa msala,na mashahidi nyuzi washavuta
So muda wowote defender,toka hivi sasa itafika
Bora usepe..kuliko kupewa kesi ya mauaji
Au kesi ya kujaribu,kupora kwa kutumia mkwaju
Hakuna mwenye mzigo,waambie wenzako mme-boogie
Na wala hatuna kimango,usione mezani kinywaji
Achana na mambo ya leo,wapi tunapiga show
Pigia wenzako simu,waambie huku ni soo
Hakuna mtu wa madini,sema ni kina jaymoe
Kabla haujaishia mikononi,kwa gorvo..au you know !
Ile anaanza kuchomoka tu,polisi washawasili
Nikasikia mikono juu..kwa sauti ya ukali
Kukimbia akala ya mguu,akasalimu amri
Akanyoosha mikono juu
Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
VERSE 4 (CHIDI BENZ)
Hata police ni mdili na ndo mchongo ameupanga..
Na ndo yeye wamemtuma jukumu lake kuwa mwanga...
na ile paaahh!! Kama Suka kama kulenga mchanga
Mwisho wa siku mahesabu watu wakacheze fanga
Mchezo kamili ulishapangwa yaliyopita ni historia...
na maneno kaa ya kwenye kanga ya hesabu nishatulia
Wa kucheka wamecheka wa kulia wamelia
Nchi bado haikufea so hamtochoka kusikia
Michezo kama hii kurudia ninajua walala hoi
Wamechoka vumilia...yeeahh
Damu zitamwagika kwa wema na wasio wema...
na imani ya mkabaji ulichokimeza utakitema
Kuna movie ila maisha ka cinema
Unyang'anyi na uchukuzi unaoatokeo kila nikihema ...(hema)
Wanasema ukila nyama....lazima utake tena..
na kweli macho kwa maneno ya viongozi wanaosema
Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia
So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh
Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia
So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh

Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates