Monday, January 25, 2010

J.POP talks about his life in BONGO FLAVA...




J.POP a.k.a PROSPER.kwa jina la Pasport anaitwa James Prosper kisanaa zaidi wanamuita. J.POP yes! aka PROSPER...Mzaliwa wa Iringa pale Town.

Miaka iliyopita, elimu yake ya mwanzo aliipata shule ya msingi Ipogolo. Shule ya Secondari ya Lugalo pale pale town, na baada ya hapo tena akamaliza kidato cha tano na sita pale pale Highland Sec School Iringa town, Nasasa anamalizia elimu yake ya juu hapo Dar city, katika chuo cha biashara CBE.

Wakati huo wote anapiga book na huku anatambaa na Music ndiyo maana watu wake wanaweza kuniona kama ana beep ktk game Nooooo!.siyo kihivyo wana,ni mipango tu mizuri na hili gemu la bongo na anamshukuru Mungu amelisoma toka alipoanza mwaka 1996 akiwa na kundi lake lililotambulika kwa jina la TOIG’Z ( THE OJAA INTERNATIONAL GANGSTAR’S) Kundi hilo liliwakillishwa na wasanii wane OBK’Z , ADDO BOY ambaye kwa sas anaimba GOSPEL, A-SMOOKER , na yeye mwenyewe J.POP , walifanikiwa kufanya track kadhaa pale Iringa town katika studio za DON BOSCO, na mafanikio ya kundi yalikuja pale walipotoa track yao kupiti studi za FM STUDIO producer akiwa ni MIIKA MWAMBA KALI, mwaka 1999,track ilikuwa inaitwa ‘’SIRI YA HATARI’na zilifuatia track nyingine kama mbili, hazikupata mafanikio kivile kwani hawakutambulika kitaifa zaidi,walitambulika pale mkoani pekee.

Na mambo mengine mengine yaliwakuta kama kundi walipokuwa DAR wakijaribu kufanya harakati.Ndipo baadaye kundi likasambalatika baada ya kila mmojawao kijitosa shuleni,wana wakapiga kimyaaaaa!...ndipo akaondoa ukimya , sana tu watu wa Iringa wanamsoma na anawakumbusha mbali kipindi ambacho makundi makubwa pale town kama EMERGENCE POISON, CRAZY DOGG, DOWN LOW, DANGEROUS CREW, kundi ambalo MIKE TEE alikuwapo, SQUIZER, GEEZ MABOVU zamani kama MED, B-BOY, DATAZ, ZAY ‘B’, na S.O.G kundi ambalo AY’, SNARE zamani aliitwa ADAM, pamoja na BUFF G’ zamani aliitwa GEMBE walikuwa wanaunda kundi hilo wakiwa wanasoma huko, Na makundi mengine kibao lakini hayo ndiyo anayoyakumbuka.

kulikua na ushindani wa kufa mtu enzi hizo. Na baada ya hapo ndipo akaanza kutoka mmoja baada ya mwingine, mpaka hivi sasa. Ndipo akajitokeza J.POP mwaka 2002 ngoma yake ya kwanza kwa marehemu ROY mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amen, haikufanya vizuri ikabuma akatoka na ngoma yake ya pili mwaka 2005 Ikaanza kusikika mwaka 2006, Track ’TUNAKUPENDA’’(unaweza kuisikiliza ktk playlist hapo) iliyotengenezwa pale JAG RECORDS producer JONAS, na baada ya hapo mwaka 2007 mwishoni akatua kwa AMBANGIRE pale home kwao IRINGA na kushuka na ngoma yake heeeeavy ‘’NITAWEZA’’ upande wa chorus ameketi RAMA DEE ambayo mpaka sasa ndiyo iliyopo na video yake pia imetenenezwa na KALAGE ,ana sema Sorry kwa washabiki wake wamekuwa wanakerekwa na kukaa muda mrefu kwa track baada ya track.Wasikonde mambo ya Shule kidogo wana , lakini HIP HOP ndivyo inavyotakiwa kwenda watu wapate muda wa kuisoma track moja na nyingine tuzipe muda nyimbo zetu. AU!!!!!


Ok Basi hivyo hivyo! Malengo yake nikutoa track za ukweli moja baada ya moja ambazo kila moja itakuwa na uwezo wa kujibeba kama ilivyo, kujirekebisha kwa kila ngoma inayokuja kutokana na mawazo na michango ya mashabiki wake, Kaeni tayari kuna ngoma itakuja hivi karibuni .


Wapo wale waliochangia uwepo wake na angependa kuwashukuru... kwanza Mungu wake, Wazazi wake RIP mama yake" MOM, I know ananisikia huko na wote wanaoniona na kunisikia Pamooja sana".ALL ABOVE IS HIS SHORT STORY***** IRINGA STAND UP’’ ukanda wa juu ISHI HIP HOP.......

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates