Friday, May 28, 2010

ASEMAVYO MDAU>>>>>>>

KIPINDI CHA PLANET BONGO EATV CHAPOTOSHA UMMA(Pt I)

na>>>>>>>RENATUS KILUVIA

(http://muzikinamaisha.blogspot.com/)

Wadau habari zenu,naamini hali zenu ni njema kabisa na ujenzi wa taifa unaendelea kama kawaida,leo nina mengi sana ya kuzungumza juu ya yale yaliyonikera,kama wiki tatu sasa nimekuwa karibu sana na kipindi cha PLANET BONGO cha EATV nikikifuatilia kwa ukaribu zaidi.Kwa wale wafuatiliaji wa kipindi hiki wiki hizi tatu kipindi kilikuwa kinarusha exclusive toka Mwanza(Rock City) pamoja na Arusha(A-Town).Kutokana na hilo nimepata nafasi ya kugundua kitu, kipindi ambacho mtangazaji wa PLANET BONGO Abdalah alikitengeneza Mwanza ni wakati alipopata nafasi ya kwenda kwenye show ya mwanamuziki wa Nigeria J-Martins iliyofanyika jijini humo hivi karibuni na kile kipindi cha Arusha hakukitengeneza yeye,bali alichukuwa kipindi ambacho kilitengenezwa na mtangazaji mwingine wa kituo hicho Bhoke Egina aliyekuwa anafanya kipindi cha 5 CONNECT wakati huo na kilikwishawahi kutumika kabla ndani ya kipindi hicho cha 5 CONNECT.
               Kilichonisukuma kuandika makala haya ni muendelezo ambao Abdalah aliufanya na kunitatiza,sijui idea hii aliipata wapi,napata shaka kuwa mtangazaji huyo halikuwa kusudio lake la kwanza kufanya hivyo wakati anatengeneza kipindi hicho,nadhani ni idea ambayo ilikuja katikati kabisa na inawezekana ilikuja wakati tayari sehemu ya kwanza ya Mwanza na ya pili ya Arusha imeshakwenda hewani,na kilichofanyika ni ”ilimradi” kipindi cha wiki ya tatu kipatikane ili wiki ipite,hii si dalili nzuri kwa crew nzima ya kipindi pamoja na mtangazaji huyo aliyepatikana toka katika mchakato mrefu na mgumu uliohusisha vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakiiwania nafasi hiyo mwaka juzi.Kipindi cha PLANET BONGO cha wiki hii ya tatu kilifanywa kwa kulinganisha mikoa hii miwili iliyotumika kutengeneza vipindi vilivyopita(Mwanza na Arusha),kwamba wapi kuna muziki zaidi?Mwanza au Arusha?na wengi waliopata nafasi ya kuzungumza ni wafanyakazi wa EATV,nilipata nafasi ya kumtambua Dj Kim na maproducer wa vipindi mbalimbali vya kituo hicho,na wote walitoa tathmini kutokana na kile kilichofanywa katika vipindi vilivyopita.Yalizugumzwa mengi lakini mwisho wa siku aliyekuwa akitazama kipindi aliweza kupata matokeo japo hayakutangazwa,Arusha ilionekana INA MUZIKI zaidi ya Mwanza,chimbuko la muziki wa HIPHOP lilionekana Arusha.
                 Kuna mwanafalsafa mmoja alikwishawahi sema “NO RESEARCH,NO RIGHT TO SAY” akiwa na maana “BILA TAFITI,HAKUNA HAKI YA KUSEMA”,kitu ambacho crew ya kipindi cha PLANET BONGO imekifanya,crew hiyo imesema bila kufanya utafiti wa kutosha,binafsi sidhani kama hawa jamaa walikuwa na haki ya kulinganisha kimuziki mikoa hiyo miwili kwa kutumia “tuvipindi huto tuwili” walitotutengeneza.Mimi ni mwenyeji wa Mwanza,nimezaliwa Mwanza,nimekulia Mwanza,kwahiyo Mwanza naijua vizuri na muziki wa Mwanza naujua vizuri sana(hakuna anayeweza kunidanganya).Binafsi nimekuwa mdau wa muziki Mwanza tangu napata akili za kiutu uzima,nimefanya kazi kama mtangazaji wa redio zaidi ya moja kanda ya ziwa na nimekuwa niki-deal na muziki huo kanda ya ziwa kwa zaidi ya miaka nane, ndo maana nimeamua kuzungumza haya,naamini Mwanza kuna MUZIKI zaidi ya kokote TANZANIA hii,utafiti huo nimekwisha ufanya japo si utafiti rasmi,nina utetezi na sababu nyingi na za msingi za kusema hivyo,naomba nianze kutoa utetezi wangu kwanza kutoka katika vipindi hivyo vya PLANET BONGO vilivyorushwa.
ENDELEA KUKODOA MACHO...ITAENDELEA>>>>>>>

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates