Thursday, September 16, 2010

KIDBWOY AVAMIWA NA JAMBAZI(15-09-2010)

SANDU GEORGE MPANDA(KIDBWOY)
Mtangazaji na dj wa Radio Free Africa na Producer wa TETEMESHA RECORDS KIDBWOY amevamiwa na mtu nyumbani kwake jana tarehe 15-09-2010 na kupigwa ikiwa ni pamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani…kwamujibu wa habari niliyopokea toka kwa mtangazaji mwenza wa KIDBWOY ajulikanae kwa jina la SKY WALKER,amesema KIDBWOY ameumizwa na hayuko katika hali nzuri na hapa ninukuu sms niliyo pokea toka kwa SKY WALKER(Kid amevamiwa jana kwake mida ya jioni na mtu anayedhaniwa kuwa ni msanii, amemjuruhi vibaya kwa kumchoma na bisibisi maskioni na kumpiga na kitu kizito kichwani, yuko Bugando Hospital wodi namba C 603 ghorofa ya 6, hali yake si nzuri sana...),tutaendelea kuwajulisha mambo yanavyoendelea na twaomba ushirikiano wenu hasa katika maombi kumuombea ndugu yetu apate kupona…

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates