Tuesday, December 7, 2010

THE NGOMA AFRICA BAND KUUANZA MWAKA 2011 NDANI YA SERBIA..

Bendi maarufu ya mziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU,wanatarijiwa kutumbuiza katika mji wa Belgrad,nchini Serbia,ulaya ya mashariki katika maonyesho ya Film and music festival yatakayoanza tarehe 5 hadi 12 January 2011,
Pia wakazi wa mji wa Montenegro watavamiwa na muziki huo wa dansi kutoka kwa ffu wa Ngoma Africa band yenye maskani yake nchini Ujerumani.
Ni juzi juzi tu wakali hawa wa mziki wa dansi na "MZIMU WA MZIKI" walikuwa wakipeperusha CD maalum "Jakaya Kikwete 2010" ambayo waweza ipata kupitia blog hii...
Toka bendi hiyo ipelekewe mwaliko wa kwenda SERBIA ,wanamziki wa bendi hiyo wamshikwa na matumbo joto! kutokana
historia ya nchi ya SERBIA ambayo miaka ya nyuma ilikuwa na vita....Pia ziara ya wakali hao Ngoma Africa band,ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kwenda Serbia

wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates