Thursday, May 26, 2011

C-SIR MADINI-KIFUNGO HURU

Sisi kama TETEMESHA RECORDZ tumejiwekea malengo ya kuwa tunajaribu kutafuta wasanii wachanga kabisa lakini wenye vipaji na kuwapika kisha kuwatambulisha katika music industry hapa TZ.
Tulianza na HUSSEIN MACHOZI, akafuata SAJNA na sasa ni zamu ya msanii mwingine mpya C-SIR MADINI kutoka Mwanza.
Huyu tunaemtambulisha sasa jina lake kamili ni PETER MPONEJA, na jina lake lingine la nyumbani ni MASISA, hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. ila kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.


Huu ndio wimbo wake wa kwanza kutoka, na utakuwa katika album yake ya kwanza ambayo bado tunaendelea kuirekodi. Video ya wimbo huu imekwishafanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo.


SONG'S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Contacts: C-SIR MADINI: 0712-719004
               KID BWOY: 0713-131073

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates