TAARIFA KWA UMMA
Jana tarehe 8 Julai 2011 Polisi walinikamata kwa kile walichokiita kuwa ni kufanya mkutano bila kibali.Hata hivyo, mtiririko wa matukio unaonyesha kwamba polisi walisukumwa na sababu nyingine kwa kuwa suala la taarifa kupelekwa polisi kama sheria zinavyohitaji lilishashughulikiwa na viongozi wa CHADEMA mkoa na wilaya ya Mbeya Mjini.
Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘BURUDANI NYUMBANI’) ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la FIESTA pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.
Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa RUANDA NZOVWE ambao ni maarufu kama Uwanja wa Dr hilo 
Maneno na vitendo vya Jeshi la Polisi vinaelekea kuwa na uhusiano na kauli ambayo niliitoa hivi karibuni kupitia mtandao wa Facebook ya kutohitaji tamasha la Fiesta kufanyika Mbeya.
Katika mazingira haya ni muhimu nikaeleza tu kuwa kauli yangu kuhusu Fiesta ilikuwa na madhumuni ya kuanzisha mjadala kuhusiana na suala zima la wizi na unyonyaji uliopo kwenye Sanaa, ambao sio tu unawanyima haki Wasanii, bali pia kukosesha mapato kwa Serikali ambayo  yangetokana na kodi  kupitia Sanaa ikiwemo muziki.
Nilifanya hivyo baada ya tamasha hilo 
Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi  ni sehemu ya vyanzo vya maovu  kwenye maendeleo ya  muziki hapa nchini.  Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa.  Na hii ni kutokana  na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise) biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi  watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye  biashara ya muziki.
Waandaji  wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.
Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa.  Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye  Tamasha la  majahazi, Zanzibar kama  wangetumia nafasi hizo kwa haki na maendeleo ya sanaa.  Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya (“empire”) hii imetumia nafasi yake dhalimu  kukandamiza watu wengine hasa Wasanii.   Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo “himaya” yao yao 
“Empire” hii imehodhi mpaka  makampuni ya udhamini hapa nchini, ambapo makampuni haya yamekuwa magumu kutoa udhamini kwa wadau wengine kwa kuwa tu wao ni washirika wa “Empire” hii.
Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa “Wadosi” ambapo bila ya wao kuruhusu basi  Msanii yeyote kazi  yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika.  Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.
Kibaya zaidi wamehodhi mpaka  nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii.  Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii wa Tanzania yao Tanzania sana 
Vitendo hivyo wanavyofanya vimeleta madhara katika tasnia ya sanaa na   matokeo yake ni kudumaa kwa maendeleo ya muziki hapa nchini.  Vijana wengi wanaojihusisha na sanaa wamepoteza matumaini.  Wengi walipata tegemeo la ajira kupitia muziki, lakini hali haipo hivyo tena.  Vijana wengi wasanii wamekata tamaa kwa ajili ya ukandamizaji wa “empire” hii.
Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili.  Kwa watu  hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi.  Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Art  Theatres 
Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni “Mhanga” au “victim” wa uharamia wa “himaya” hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama  mwakilishi umma.
Izingatiwe kuwa  baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa  kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge.  Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi.  Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria  walianza kulipwa vizuri kama  wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.
Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira,  Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?
Wenu katika kutaka haki,
Joseph Mbilinyi (Mb)
9/7/2011-Mbeya Mjini
 






 

 
0 comments:
Post a Comment
DEE BᵘᵐZ®