Friday, August 6, 2010

NGWAIR-MIKASI

MIKASI LYRICS feat MOX,RAH P,MKOLONI
Top of Form

Verse:- I Ngwea
Ni asubuhi naamka ninapiga mswaki
Kisha naenda kubath kuweka mwili safi
Narudi ghetto nafungua kabati
Nachukua pamba blingbling kwa chati
Nna t-shirt black nna jeanz ya kaki
Na chini nina simple white chata nike
Kisha mzee najipulizia marashi
Nanukia safi
Niko na machizi wa chamber squad na Dark
Tunawapigia simu Rich Coast wako wapi
Tunakutana mitaa ya Chaga Bite
Asubuhi tunapata zetu supu kwa chapati
Na mitungi ya kupotezea wakati
Ukitaka fegi mezani kuna pakti
Iwe sm yani sports au embassy
Hapa utakula raha mpaka mwenyewe utasema basi
Tunakamua mpaka ile mida ya lunch
Tunaagiza ugali mkubwa na samaki
Makamuzi yanaendelea mpaka night
Watu wanaingia graveyard kwanza kupata nyasi
Tunarudi kila mmoja anajisachi
Ni kiasi gani mfukoni kilichobaki
Kujicheki mi nna kama laki
Nikawaambia machizi kinachofuata MIKASI

Kiitikio:- Ferouz
Mitungi,blunt mikasi{oooh yeeeaaaaaaaah}
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
rudia kiitikio x2

Verse:- II Ngwea
Kulewa tushalewa kilichobaki mikasi
Washikaji eh milupo tutapata wapi?
Milupo labda mitaa ya kati
so tunaenda vipi kwa miguu au kwa basi?
Usiku huu bora tuchukue tax
Poa basi tusiponaita tax
Njo utupeleke mitaa ya kati
Tukacheki midudu ya kupiga mikasi
Tuelewane kabisa itatucost sh’ngapi?
{4000 tu}
Aah wapi
Kwani hapa na pale ni umabali wa hatua ngapi?
{Si unacheki mwenyewe mko wangapi}
Usimind sana babake hatuko safi
Tuchangeni tusipoteze wakati
Ludigo kwani we una tshs ngapi?{buku tano}
Venture{bati} sasa we unabati usiku huu unaenda wapi
Wakati hiyo bati hata soda tu hupati
Bora huweke kesho unywee chai na chapati
Asiye na kitu mi naona bora akabaki
Tusije mbele tukashikana mashati
Suka eh! tuanzie Masaki
Mchizi kapiga simu yaani kuna bonge la party

Rudia kiitikio x2

Verse:- III Ngwea
Dereva funga break tushafika kwenye party

:-MOX

{Eeeh bwana eh kumbe bonge la party}

 :-NGWEA
Cheki mademu kibao utadhani kitchen party..

:-MOX

{Duh!cheki lile anti lililovaa skintight
Ee bwanaeh!liko safi sio mchezo babake unaweza ukahonga laki

:-NGWEA

{Aah wapi mtu kama mi hanipati
Usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati}

:-MOX

Poa basi tujichanganye katikati
Tukacheki mitungi na mademu wa mikasi

Bridge
Braza mwenye black unaitwa na yule anti
’Yuko wapi’
yule aliyevaa suti ya kaki
Anti vipi?

(Rah P)
Aah safi samahani kwa kukupotezea wakati
Nilikuwa naomba tuwe wote kwenye party
Au unasemaje?:

(Ngwea)
Mi naona safi

(Mchizi Mox)
Samahani wewe anti ambaye umevaa shati
Hivi unaitwa nani eh?}:naitwa Bahati:
Hivi anti nishawahi kukuona wapi?

(Rah P)
Acha longolongo we sema una sh’ngapi
Oyaa we vipi mpango wako vipi?

(Mchizi Mox)
Mbona mi mazee mpango wangu safi
Ishakuwa usiku twenzetu tukachukue tax
Twenzetu tukapige mikasi

Rudia kiitikio x2

Verse:- IV
Eebwana eh niko arround mazee
Rudia kiitio x2

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates