Sunday, September 5, 2010

ROMA-PASTOR LYRICS

ROMA
INTRO…..
Yeeeah  waacheni  watoto  wadogo waje  kwangu….
Maana   ufalme  wa  mbinguni  ni  wao
j..ryder  where  you  ‘t?
am  the  pastor  of  this  church(times  2)
am the…….it’s  tongwe  records

VERSE….1
Fanya  ishara  ya  msalaba  upokee  haya  mahubiri
Mimi  ni  mteule  ninawaletea  injili
Nina  ushuhuda  wa  kiroho  bwana  yuaja  msubiri
Natangaza  upako  na  habari  za  mnara  wa  babeli
Wachungaji  wanalumbana  wakigombania  waumini
Wanalala…wakiamka  wanaanzisha  dini
Hawaogopi  damu  ya  msalaba  bible  wanaifanya  biashara
Wewe  sio   yesu  hata  kama  baba yako  ni  fundi  seremala
Wewe  ni  nani  usiyekosea  kila  unaye  muombea  anapona
Hatutaki  shuhuda  za  uwongo  aminini  nyote  mtachomwa
Ndani  ya  vazi  la  suti  unakebehi  wakatoloki
Mtaleta  dini  zote  ila  RC  itabaki
Hata  kristo  alipoponya  hakutaka  malipo
Akaunti  yako imejaa  sadaka  zetu  wakristo 
Toba  yako  haijaswii  halafu  unajiita  una  upako
Siyo  kila  atakaye  niita  bwana  basi  ataiona  pepo

CHORUS….
We ni nani unayejiita nabii kwenye jamii
hizi nyakati za mwisho soon atashuka masihi
piga magoti tusaaaaliii  !!! Ameeen…..!!!
piga magoti tusaaaaaliii !!!Ameeen….!!!
Waumini wamekimbia kanisa madhehebu yanaongezeka
hizi nyakati za mwisho cheki manabii wa uwongo
mwana wa adam yuaja…. Ameen !!!
 mwana wa adam yuaja …Ameen!!!


VERSE…2
 Laiti  ningeweza   ningekugeuza  jiwe  la  chumvi
Vipi  unipangie   sadaka  pastor  gani  we  mlanguzi
Hakika   ilinenwa  usitumikie   mabwana  wawili
Siasa  na  kanisa  kama hadithi za  kaini na  abeli
Kama  wasabato  wasiokula  kitimoto  wala  kambale
Wanasadaki  mbele ya  haki  wanaamini  agano  la  kale
Mnatangaza  ufahari  wenu  kwenye  vikapu  vya  sadaka
Hakuna  sadaka  ya   kweli  kama  ya  kumchinja  isaka
Kanisa  lako  halifanani  na  ufalme  wa  yehova
Madhehebu yanajitenga  kama   makundi  ya  bongo  fleva
Heshima  ya  mkatoliki  inashuka  kama  theluji
Dini  mnaifanya  miradi  kwa  kivuli  cha  uchungaji
Kanisani  mnaonyeshana  ufahari  wa  kuvaa  bazee
Hekalu  mnalichafua   kwa   sadaka  ya  pedeshee
Biblia hujaimaliza  unataka  uzima  wa  milele
Usije  ukatuchoma  moto  kama wafuasi  wa  kibwetere

Verse…3
 Hizi   nyakati  za  mwisho  soon atashuka  masihi
Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii
Kukataza waumini wasivae mapambo kwako jadi
Ili pesa wakupe sadaka na kisha unafanya mtaji
We mchungaji umekusanya waumini kwenye vijiji
Ukawaongoza sala ya toba kama yohana mbatizaji
Unabeba gunia la dhambi na yesu kumvika taji
Usiniwekee mkono kichwani huna karama ya uponyaji
Imani yako ndogo kama punje ya haradani
Uza mali zako zote pesa uwape masikini
Unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa
Haleluya haleluya kumbe unatuibia sadaka
Yesu hakuwa mganga wa kienyeji  Japo alimponya kipofu
kwa tope la mate yake ila kwako napata hofu
ee mungu napiga goti  hiki kikombe  kiniepuke
mwana wa adam yuaja basi tungoje ashuke

 OUTRO
Angalieni  mtu  asiwadanganye…maana  wengi  watakuja  kwa  jina  langu wakisema
“mimi  ni  kristo”   nao  watadanganya   wengi   haleluya…!!!  Ameeen….!! manabii wengi  wa  uwongo  watatokea,   kutakuwa na  dhiki  kubwa  siku  hiyo…jee hamsadiki  yakuwa  hizi  ni  ishara  kwamba mwana  wa  adam  yuaja…..Ameeen!!  basi  kesheni  mkisali  maana  hamjui  saa wala  siku
Am  the  pastor  of  his  church…am  the….its  tongwe  records…..

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates