Friday, June 17, 2011

THE NGOMA AFRICA BAND YAKISANUA HEIDEBERG CITY....

FFU wa Ngoma Africa band jukwaani Heidelberg City,25-06-2011
  Pia 26.06.2011 Live ndani ya Africa Tage festival,Freudenstadt, Ujerumani

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" almaarufu FFU,
imejikuta katika mshike mshike usio na mwisho uko nchini ujerumani..kwani bendi hiyo
inaparamia jukwaa la AFRIKA DAYS Festival siku ya jumamosi 25.06.2011 kuanzia saa 3 usiku
katika mji wa Heidelberg,Ujerumani, ambako washabiki wa miji ya Heidelberg,Mennheim,n.k watajirusha
na gwaride la mziki wa FFU ndani ya ukumbi Karlstorbahnhof,mjini Heidelberg.
Jumapili ya 26.06.2011 Kikosi kazi Ngoma Africa band aka FFU watatumbuiza katika onyesho lingine kubwa
la  "Afrika Tage" litakalofanyika mjini Freudenstadt,kusini mwa Ujerumani,ambako nako kutakuwa na pata shika
nguo kuchanika kati ya washabiki na "Bongo Dansi".
FFU pia wameongeza Dozi la nguvu katika kambi yao www.ngoma-africa.com ambako nyimbo za "Rushwa ni adui wa haki" na lile sebene la "Amiri Jeshi Mkuu" zinaweza kusikika.
Zogo la "Baba wa kambo" bado linaendelea at www.ngoma-africa.com  jipe raha mwenyewe
**********************************
Lile song lililojipatia umaarufu katika kila kona "Rushwa ni Adui wa Haki" kutoka kwao Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani yake Ujerumani,sasa wimbo huo umetua na unasikika katika kambi ya FFU www.ngoma-africa.com .song hilo lenye ujumbe muhim kwa jamii ni utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja, wa FFU
ughaibuni.
wimbo huo wenye mistari mitatu mitamu na mingine ya uchachu lakini yote ina umuhimu wake kwa jamii...,unasikika at www.ngoma-africa.com 

Pia kikosi cha Ngoma Africa band kitumbuiza jukwaani jumamosi 25.06.2011 mjini Heidelberg, na Jumapili 26.06.2011 mjini Freudenstadt,huko Ujerumani.
wasikilize FFU at www.ngoma-africa.com

0 comments:

Post a Comment

DEE BᵘᵐZ®

Template by:
Free Blog Templates